Sunday, December 1, 2013

TFSA Yashiriki Shughuli za Shamba la Miti.

TFSA Siku ya Leo tar 30 Nov Imeshiriki Shughuli za Shamba la Miti lililopo Karibu na Bwawa la Mindu Mjini Morogoro.
Shughuli hiyo iliyohusisha Kuondoa Magugu imefanyika na Wanachama zaidi ya 50 Kuanzia mwaka wa Kwanza wa Masomo mpaka Mwaka wa Tatu kwa Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza Ya Misitu katika Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Morogoro.
Katika Shughuli hiyo imebainika Kua Miche mingi ya Miti aina ya Albizia spp haikuweza kukua ipasavyo kutokana na Wadudu waharibifu eneo hilo.

Vilevile imebainishwa kua Shughuli za Kilimo za Wananchi eneo hilo zinachangia kusababisha miti hiyo kutokua kwani wananchi hao hawapo makini wakati wa Kulima Mazao yao kupelekea Kukatwa kwa Baadhi ya Miche.
Katibu wa TFSA Bwn Yohana Jumanne akitoa Maelekezo kabla ya Zoezi kuanza.



Wanachama Wa TFSA Wakishiriki katika Zoezi hilo.
M/kiti wa TFSA Bwn Sikoi akiwapongeza wanachama wa TFSA Baada ya Zoezi kukamilika
Wanachama wa TFSA Walioshiriki zoezi hilo katika Picha ya Pamoja.
Baada ya Zoezi kukamilika wanachama wa TFSA walipata fursa wa Kutembelea Bwawa la Mindu



HIVI NDIVYO WELCOME FIRST YEAR PARTY-2013 ILIVYOFANA.

Leo tar 30/11/2013 Kumefanyika Sherehe ya Kuwakaribisha Wana TFSA Mwaka wa Kwanza hapa Chuoni katika PUB Ya SUASA.
Sherehe hiyo iltanguliwa na Wanachama kushiriki shughuli ya Kutoa Magugu katika Moja ya Eneo la CHUO lililo karibu na Bwawa la Maji-MINDU Hapa Morogoro.

KULIA: Prof Ngaga,Dean wa Kitivo cha Misitu na Hifadhi ya mazingira ambaye Pia ni Mlezi wa TFSA Alikua Mgeni rasimi.
Aliwasihi Wanachama kutumia Fursa mbalimbali kupitia TFSA Ili kujifunza na Kushiriki katika Kazi mbalimbali zinazoendeshwa na TFSA Kwa ajili ya Maendeleo ya Sasa na Baadae.

             





                   Wanachama wa TFSA Wakimsikiliza kwa Makini Mlezi wa Chama Prof Ngaga.



                         Baada ya Hotuba ya Mgeni Rasimi ikafata Burudani ya Mziki(Kwaito)
                Ikafatia Fund Rising kupitia Keki iliyoanadaliawa kwa UMARIDADI Zaidi.


                   Ikafika Wakati wa kupata CHAKULA Kilichoandaliwa kwa Umakini wa hali ya Juu.
                                                     Acha kabisa,ilikua raha bila Karaha!