SUA
PRIMARY PROGRAM
|
COMMUNICATION OFFICER ADRESSING
CLIMATE CHANGE ISSUES |
Siku ya tar. 8/5/2013 TFSA likwenda kufanya semina
fupi, ya mabadiliko ya tabia nchi
(Climate change) katika shule ya msingi SUA.
Semina hiyo ilikuwa ni ya darasa moja, darasa la sita lakini
pia kulikuwa na wanakikundi, kikundi cha mazingira cha shuleni hapo.
Watoa mada walikuwa ni Shaabani, Salim – TFSA GS na William
Charles – TFSA COMMUNICATION OFFICER
|
TFSA-GS
asking questions to students |
Wanafunzi hao walielimishwa yafuatayo:-
- Nini maana ya tabia nchi,
- Nini maana ya mabadiliko ya tabia nchi,
- Mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na nini?
- Athari za madiliko ya tabia nchi na
- Nini kifanyike ili kupunguza tatizo hilo la mabadiliko ya tabia nchi
Wanafunzi walishiriki semina vizuri kwa kuchangia katika baadhi ya waliyokuwa wanayafahamu na pia walishiriki kwa kujibu maswali na wanafunzi waliojibu maswali vizuri walizawadiwa daftari na peni. Wanafunzi hao ni Muhati, Asheri, Eriki, Magomola, Hamisi, Charles, Shangwe, Petronila, Ester na Agness.
|
wanafunzi wa shule ya msingi SUA |
|
MSHIRIKI AKIPEWA ZAWADI
SUA TV RECORDING PROGRAM 2
Tarehe 10th May 2013
tuliendelea na program ya kurekodi vipindi mbalimbali vya kuelimisha jamii
katika kituo cha televisheni, SUA-TV. Mara hii tulizungumzia mada ya kilimo
mseto (Agroforestry)
Washiriki katika program hiyo
walikuwa, Mauki, Dickson-3rd year., Msangi, Joyce-3rd
year., Milkajane, Sangiwa-2nd
year na Samweli William Sikoi
Kipindi hicho kihusu mada ya
kilimo mseto ambapo yafuatayo yalizungumziwa;
1.
Kilimo mseto ni nini?
· Maana ya kilimo mseto?
· Mifano ya maeneo katika Tanzania yanayofanya kilimo mseto
· Kwanini maeneo hayo yanatumia njia hiyo ya matumizi ya ardhi?
2.
Kuna mifumo mingapi ya
kilimo mseto?
· Taja idadi ya mifumo iliyopo
· Elezea kwa undani kila aina ya mfumo ulioutaja hapo juu
3.
Faida ya kutumia kilimo
mseto kama matumizi sahihi ya ardhi.
4.
Changamoto zinazokabili
kilimo mseto
Ushauri kwa jamii wenye uhaba wa
ardhi na wasiokuwa na uhaba wa ardhi
|
No comments:
Post a Comment